Saikolojia ya Mteja
by Joel A. Nanauka
About this book
Taasisi ya Clarabridge iliwahi kufanya utafiti uliohitimisha kuwa 45% ya wateja ambao walihudumiwa vizuri na kuridhika na huduma/bidhaa walikuwa tayari kulipa zaidi bila ugumu wowote. Huduma nzuri kwa mteja ni hakikisho la kuongeza mauzo yako ya kila siku na kupanuka kwa shughuli unayofanya. Moja ya changamoto ya watu wengi ni kujua mbinu zinazopaswa kutumiwa ili kumfanya mteja afurahie na kuridhika na huduma ambazo unampatia. Hata hivyo ili kujua ni namna gani umhudumie mteja wako, ni muhimu sana kujua aina ya mteja ambaye unamhudumia. Kupitia kitabu hiki utajifunza aina 10 za wateja, changamoto zao na jinsi ya kuwahudumia. Hii itakusaidia sana kujihakikishia unapata wateja wengi, unawaridhisha na pia unaongeza wateja wengine. Karibu tujifunze pamoja.
What you'll learn
- 04. Utangulizi
- 05. Saikolojia Ya Mteja
- 24. Mteja Huwa Ananunua Nini?
- 57. Aina 10 Za Wateja.
- 87. Jinsi Ya Kukabiliana na Malalamiko Ya Mteja.
- 103. Hitimisho.
- 109. Kuhusu Mwandishi.
